Friday, 14 October 2011

KUYEYUKA KWA MENO (TEETH EROSION)

Na Dr. Augustine Mbehoma Rukoma
Ziko aina mbali mbali za kulika kwa meno kulingana na nini kinasababisha tatizo. Aidha kinga au tiba hutegemea nini kinasababisha tatizo hilo. Leo nitaongelea aina nyingine ya kulika kwa meno
Kuyeyuka kwa meno (tooth erosion) ni kulika kwa meno kunakosababishwa na kemikali hasa tindikali. Tindikali inayoyeyusha meno haya yaweza kutoka nje au ndani ya mwili wenyewe.
  • Kuyeyuka kwa meno kunakosababishwa na tindikali toka nje ya mwili: Baadhi ya vyakula na vinywaji tunavyokula na kunywa vina kiwango kikubwa cha tindikali (acid), hivyo vyakula na vinywaji hivyo vikikaa kinywani kwa muda huweza kusababisha meno kuyeyuka. Kiwango cha uharibifu kinategemea mara ngapi unatumia vyakula/vinywaji hivyo, kiwango cha tindikali katika vinywaji hivyo na muda vinaokaa kinywani. Tindikali nyingine inaweza kupatikana katika hewa hasa maeneo ya viwanda vinavyotengeneza betri. Myeyuko unaotokana na tindikali ya nje huathiri zaidi sehemu za nje za meno (buccal or facial surfaces).  


 kuyeyuka kwa kweno kunakotokana na vinywaji vyenye tindikali

Watu walio katika hatari zaidi ya kupata tatizo hili ni wale ambao hunywa vinywaji vyenye kaboni kwa wingi (carbonated drinks), juice ya limau au wale wenye tabia ya kufyonza limau. Tatizo linaongezeka kwa wale wenye tabia ya kuweka juice na kukaa nayo mdomoni kwa muda bila kuimeza (unaisikilizia utamu mpaka kwenye kisogo). Unashauriwa unapokunywa juice hizi kumeza haraka.myeyuko utakanao na vinywaji vyatindikali
  • Kuyeyuka kwa meno kunakosababishwa na tindikali toka ndani ya mwili: Kuyeyuka huku kunasababishwa na tindikali kutoka kwenye tumbo. Meno yanakwanguka sehemu za ndani (palatal and lingual surfaces) kama picha inavyoonesha hapa kulia.

                    kuyeyuka kwa meno kunakosababishwa na tindikali toka ndani ya mwili


Watu watu walio katika hatari kubwa ya kupata tatizo hili ni wale ambao wana matatizo ya kutapika mara kwa mara kama ugonjwa sugu na wale ambao hula sana lakini kwa vile wanataka wabaki wembamba (slim), kila wakila baada ya muda hujitapisha ili wasinenepe. Matapishi huja na tindikali iliyoko tumboni (gastric hydrochloric acid). Wanywa pombe kali sugu nao hawaachwi nyuma, pombe kali hukwangua kuta za tumbo na kusabisha chronic gastritis hali ambayo tindikali huwa inamwagika kwenye tumbo zaidi ya kawaida na wakati mwingine hurudi kinywani kama mvuke na kusababisha madhara haya.

Hali inakuwa mbaya kwa wale wanao tapika mara kwa mara na katika hali ya kurudisha maji mwilini maana wanakuwa na kiu ya mara kwa mara hunywa juice au soda kwa wingi pia ili kukata kiu. Watu wa aina hii meno yao huyeyuka sehemu zote yaani nje na ndani.
Dalili
Katika hali zote eneo lililoathirika huonekana angavu, gumu, la njano kuelekea kahawia na laini (smooth).
Dalili zake ni kama zile za kulika kwa meno kunakotokana na namna nyingine, msisimko (sensitivity) wakati wa kunywa vinywaji baridi, kuvuta hewa na hata maumivu kulingana na kiwango cha uharibifu na uwezo wa mwili kujihami.
Matibabu

Matibabu hulenga kugundua na kutibu kisababishi. Kama ni matatizo ya tumbo tabibu wa meno atakupeleka kwa tabibu wa kawaida (general practitioner/physician). Kwa wale wenye tabia hatarishi, la msingi ni kushauriwa kuacha tabia hizo. Mgonjwa akitengemaa basi sehemu zilizoathirika huweza kupigwa viraka kwa dawa zenye rangi kama ya jino (composite veneer).
Kwa wale walioshindikana meno huvalishwa kofia ngumu (crown) ili kuyakinga na myeyuko zaidi.

Kuoza kwa meno (Dental Caries) ni ugonjwa wa kuambukiza

Dr. Augustine Mbehoma Rukoma 
Miaka ya nyuma iliaminika ugonjwa wa kuoza kwa meno si wa kuambukiza; lakini tafiti nyingi zilizofanyika zimethihilisha ni ugonjwa wa kuambukiza. Jino lililooza linaweza kuambukiza meno yaliyogusana nalo na pia mgonjwa aliyeoza meno au mwenye wadudu wanaosababisha kuoza kwa meno anaweza kuambukiza mwenzake/wenzake.
Wadudu wanaosababisha kuoza kwa meno ni sehemu ya wadudu wakazi kinywani (oral flora). Wadudu hawa hujishikiza kwenye meno na kufanya utando, wana uwezo wa kuchachua vyakula hasa vyenye asili ya sukari na kutoa tindikari. Ni tindikali hii ambayo huvuta madini kwenye meno na kuweka matobo. Utando huu wa wadudu kwenye jino moja unaweza kuwa na wadudu nusu biliononi, miongoni mwake ikiwemo jamii ya  mutans streptococci ambao kimsingi ndio wasababishaji wakuu wa kuoza meno. Waduduwengine ni kama Lactobacillus na Actinomyces
Namna ya kuambukiza-ndani ya jamii ya wadudu hawa ziko jamii zingine ndogondogo ambazo zinatofautiana kwa uwezo kuchachua vyakula na kutoa tindikali na hata uwezo wa kujishikiza kwenye meno. Kwa mtu mwenye wadudu wasio wakali anaweza kuambukizwa na mwenzake mwenye wadudu wakali na hivyo kuingia kwenye hatari zaidi ya kuoza meno. Tafiti zimeonyesha wapenzi/wanandoa kwa njia ya kubusiana wanaweza kuambukizana kwa njia hii. Watoto wanaochangia ice cream/ice water mashuleni pia wanaambukizana kwa njia hii. Tafiti pia zimeonyesha wazazi wanaotafunia vyakula watoto wao kama sehemu ya kuvilainisha wanaambukiza pia.
Njia nyingine ni jinolililooza kuambukiza menzake linayogusana nayo, tindikali inayozalishwa na wadudu katika jio lililooza linaweza kuathili lililo jirani. Ndio maana inashauriwa ukiona jino limeanza kuoza muone mtaalamu akalitibu au akaling’oe kama alitibiki ili lisiambukize mengine.
Namna ya kujikinga-
·         Njia muhimu ni kutembelea cliniki za meno angalau kila baada ya miezi sita
·         Kuzuia watoto kuchangia vyakula mudomoni
·         Kupima kuangalia kiwango na aina za bakiteria zilizi kwenye mate yake na kupata dawa ikibidi.
·         Kuhusu kubusiana sina la kusema

KUOZA KWA MENO MENGI KWA KASI KWA WATOTO WADOGO (RAMPANT CARIES IN CHILDREN)

Dr. Augustine Mbehoma Rukoma
DDS, MDent (Restorative Dentistry)
Tafsiri  ya neon “rampant caries” ni nyingi katika fani ya meno lakini la msingi ni kuoza kwa meno kunako enea kwa kasi na kuharibu vichwa (crowns) vya meno mengi au yote yaliyoota. Hii ni hali mbaya ya kuoza kwa meno ambayo hushambulia zaidi meno ya utotoni (milk teeth or primary dentition), japo wakati mwingine hata ukubwani.
Ugonjwa huu unajidhihilisha kwa kuanza na kuongezeka kwa kasi na kwa namna unavyo yashambulia meno na vyanzo vyake. Meno ushambuliwa kwa mpigo hasa kuanzia meno ya juu mbele, meno ya chini mbele ni mara chache kushambuliwa kwa vile yanakingwa na visababisha vya kuonza na ulimi.  Ugonjwa huu ushambulia hata maeneo ya meno ambayo kwa hali ya kawaida si rahisi kuoza, kama sehemu ya kukatia kwa meno ya mbele (icisal edges) na sehemu ya mbele kati na nyuma kati (facial and lingual surfaces).
Vijino vilivyo athilika uonekana brauni au vyeusi kama mkaa


 meno yaliyooza kwa wingi na kwa kasi yakiwa na rangi nyeusi
     meno yaliyooza yakiwa na rangi ya brown      
Nini husababisha meno kuoza kwa kasi utotoni?
Nadharia nyingi zinaonyesha kuna uhusiano mkubwa kati ya ugonjwa huu na tabia ya ulaji ya mtoto (feeding habits). Mfano kisababishi kikubwa ni watoto kunywa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na mara nyingi kwa kutumia chupa za kufyonzea (nursing bottles) ndio maana ugojwa huu wakati mwingine huitwa nursing bottle caries. Hii hujitokeza haswa kwa watoto wanaochwa na yaya zao, ambao huwapa vinywaji hivyo kila wanapohitaji au wakilia. Pamoja na kwamba ugonjwa huu hutokana zaidi na chupa za kufyonzea, japo mara chache lakini pia yawezekana kutokana na mama kumnyonyesha mtoto mara kwa mara au tuseme kila anapo hitaji; vile vile wale akina mama ambao hawataki usumbufu usiku hivyo kutumbukiza nyonyo zao kwenye vinywa vya watoto na wao kujilalia, hapa mtoto hujinyonyea usiku kucha hali hii kitaalamu hujulikana kama at will breast feeding.
Watoto walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu
·         Watoto wa masikini ambao hawapigi mswaki kwa kizingizio cha kwamba mtoto ni mdogo, kumbuka meno ya utotoni yana madini kidogo
·         Watoto wa wafanyakazi wanashinda maofisini wakati wa kunyonyesha na waacha watoto kutumia chupa za kufyonzea kwa muda mrefu ambao hawapo nao
·         Watoto wagonjwa sugu wanaotumia dawa zenye sukari (syrups) mara kwa mara.
·         Watoto wanaoachwa kunyonyeshwa mapema na hivyo kutumia chupa kama  mbadala

Namna ya kumkinga mtoto wako
·         Punguza matumizi ya chupa za kufyonzea
·         Msipende kuwanyonyesha watoto kila wanapotaka hivyo, hasa kunyonyesha inapotumika kama njia ya kupoza mtoto anayelia
·         Jenga tabia ya kuwakagua watoto vinywani mara kwa mara na ukiona tatizo mpeleke hospitali mapema
·         Wasaidieni watoto kupiga mswaki mara baada ya meno kuanza kuota
·         Dhibiti matumizi ya vinywaji na na vitu vya sukari mara kwa mara
·         Msipende kuwapa watoto wadogo fedha kwani matumizi yake ni pipi na ice water au vinavyo fanana na hivyo
Matibabu
·         Kuziba meno yanayoweza kuzibika
·         n’goa yanayouma na hayawezi kuzibika na kutumia vitunza nafasi (space maintainers).
·         Acha yasiyoweza kuzibika lakini hayaumi yatatoka wakati wake ukifika
·         Pakaza madini ya fulolini kwa watoto walio katika hatari kubwa



mtoto akifyonza chupa

Wednesday, 12 October 2011

KUYAFANYA MENO YENYE RANGI KWA MEUPE

Na Augustine Mbehoma Rukoma-DDS, MDent (Restorative Dentistry)
Wakati wa mwongo uliopita mahita ya kuboresha muonekano au kulembesha meno yameongezeka kwa kiwango kikubwa hasa katika nchi zilizo endelea, hii imechochewa na kupatikana chemikali za meno mpya (dental meterials) na vifaa kwa kasi ikiendana na kuboresha vile vya zamani. Sehemu nyingine iliyosababisha madaktari na mainginia wa meno ku
kuyafanya meno kuwa meupe ni se hemu ya fani ya taaluma ya meno chini ya ulembeshaji wa meno, fani hii jihusisha na boresha muonekano wa meno hasa hasa yale yanayo onekana wakati wa kutabasamu na kuongea. Inahusisha matibabu kama kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe, kunyoosha meno yaliyojipanga vibaya pamoja na kukarabati meno yaliyovunjika na yale yaliyoumbika visivyo (malformed teeth). Huko uingereza na sehemu nyingine za magharibu wanawake waliowengi wanatumia maelfu ya paundi/euro kuboresha mwonekano wa meno yao ali ambayo na huku inaanza kuingia
 Nini husababisha meno kugeuka rangi?
Meno kugeuka rangi husabishwa ni kimojwapo au muunganiko wa vitu vifutavyo: -
1. Vyakula na vinywaji kama vile vinyaji vyenye kaboni, wine na sigara.
2. Utumiaji wa maji yenye kiwango cha juu cha madini aina ya magadi (fluoride)  na utuumiaji wa magadi katika kulainisha vyakula katika kupika vyakula vigumu kama maharage na makande. Utafiti uliofanyika tanzani na Prof. Mabelya na wenzake umeonyesha kuwa kubadilika kwa rangi kutokana magadi kwa kiwango kikubwa ni kutumia magadi katika mapishi  ya vyakula hasa makande kule moshi kuliko ilivyo kwa maji.
3. Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ngumu za jino (enamel and dentine defects). Sehemu ngumu ya meno kama imeumbwa ikiwa laini ni rahisi kufyonza rangi na jino kuuota likiwa limegeuka rangi au kugeuka baada ya kuota.
4. Matumizi ya madawa kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayajapata madini ya kutosha na hata watoto wachanga ambao meno yao hayajakomaa. Systemic drugs such as tetracycline when taken during pregnancy or early child may be absorbed developing teeth buds which are not yet or less mineralized. 5. Kufa kwa kiini cha jino hasa kutoka na kujigonga wakati wa ajari au kupigana ngumi usoni (pulp necrosis), jino likigongwa mkwa nguvu damu huvuja ndani ya kiini cha jino na baadae huchachuliwa na kuto chemikali ambayo hupenya kwenye vitundu vidogo vodogo kwenye dentine na kujidhihilisha kama brown, zambarau au hata nyeusi. Hali hii yaweza tokea mapema baada ya kupata ajari lakini wakati mwingi inaweza kuchukua miaka kadhaa hata arobaini wakati mtu hakumbuki kuwa alitwangwa ngumi.

Kuyafanya meno yenye rangi yasimpendeza mwenye nayo kuwa meupe
(Bleaching or teeth whitening)
Kuhu ni kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe au kuongeza weupe wa yale yenye rangi ya kawaida kufikia kiwango cha weupe atakacho muhitaji kwa kutumia chemikali maalumu. Rangi ya kawaida ya meno kwa walio wengi ni uweupe kama wa maziwa (milky white). Rangi yeyote nje ya hiyo ni si ya kawaida (abnormal color or discoloration).
Kuwa na rangi isiyo ya kwaida hasa kwa meno ya mbele linaweza kuwa tatizo kubwa la urembo na kumsumbua mhusika kisaikolojia. Kuyafanya meno kuwa meupe kumelenga kuwaondelea wahusika tatizo hili japo mafanikio yake yanategemea kiwango rangi isiyo ya kawaida.
Kufanya meno kuwa meupe kwa kutumia chemikali, kunaweza kubadili yaliyo na rangi isiya ya kawaida kutoka yale yaliyoathilika kwa kiwango kidogo mpaka cha kati.  
Kufanya meno yawe meupe kwa kutumia chemikali uunguza (ixidises) rangi na kuiondoa. Chemikali zinazotumika   zina hydrogen peroxide 30%-35% na baadhi carbamide peroxide 10%. Chemikali hizi huweza kuondoa rangi zilizo sababishwa na vyakula, vinnywaji dawa za tetracycline, rangi kidogo iliyotokana na utumiaji wa madini ya magadi kwenye vyakula au kwenye maji (mild fluorosis) na mmeno yenye rangi ya yellow au grey itokanayo na umri kwenda. Inaweza kuondoa rangi itokanayo na uvutaji wa sigara na matumizi ya ugoro. Kwa wavutaji wa sigara sharti waache watumiapo chemikali hizi kwani muunganiko hydrogen peroxide na chemikali zilizopo kwenye moshi wa sigara unakisiwa kuongeza madhara ambayo tayari moshi wa sigara unasababisha kwenye mwili wa binadamu. Akina mama wanaonyosha haishauliwi pia pamoja na kwamba hakuna madhara ambayo yanajulikana mpaka sasa. 
kuboresha weupe wa meno kutumia chemikali


Kupiga meno viraka (Veneering)
Hii hufanyika kwa kuondoa sehemu ndogo ya juu ya jino kwenye enamel kama 0.5-1mm na baadae kupandika dawa yenye rangi nyeupe kulingana na mgonjwa anavyotaka mwenyewe.
Picha sikonyesha meno yaliyobadlika rangi kutokana na magadi kabla na baada ya kupigwa viraka


picha ya juu, meno yaliyoathilika na magadi kabla ya kupigwa viraka wakati ya chini ni baada ya kupigwa viraka (veneer)

Kumbuka: kuna rangi zaidi ya 26 nyeupe ambazo miongoni mwake mgonjwa anaweza kuchagua anayoitaka