Tuesday 8 November 2011

Watu wengine wanaweza kuwa na wenza wenye ukimwi bila kuambikizwa kwa muda mrefu au hata wasiambukizwe kabisa-taarifa (case report)

Na Dr. Augustine Mehoma Rukoma
Utangulizi
Neno ukimwi ni kifupisho cha maneno “Upungufu wa Kinga Mwilini”. Ugonjwa huu usabishwa na virusi ambavyo hushambulia chembe chembe za kinga na kuufanya mwili ushindwe kujilinda dhidi ya maradhi ipasavyo au hata kushindwa kupambana na maradhi yaliyoingia tayari.
Ukimwi uambukizwa kwa njia mbali kama; 1. kuingia damu ya mtu mwenye ukimwi kwa hasiye nao-hapo ndo kuna vitu kama kuchangia nyembe, sindano, kuwekewa damu isiyo salama n.k. 2. Kujamiiana- wadudu wa ukimwi wameonekana kuwemo kwenye majimaji ya sehemu za sili, hivyo kama kuna michubuko mtu akafanya tendo hili na mhadhilika kuna nafasi ya kuambukizwa. 3. Mama mjamzito kumuambukiza kiumbe kilichopo kwenye mfuko wakewa uzazi.
Japo si jukumu la makala hii lakini kinga ni pamoja na kuzuia kuchangia vifaa vyenye ncha kali, ktumia kinga unapofanya tendo la ndoa, kuacha kufanya tendo la ndoa kama unaweza na mengine.
Kwa vile kuna uwezekano wa kupata ukimwi kwa kutenda tendo la ndoa, wanandoa ambao kimsingi wengi wao kama si wote, hawatumii kinga wanapofanya tendo hili. Katika hali hii, kama kuna uwezekano mmoja ni muathilika, basi nafasi ya kumuambukiza mwenzake uongezeka.
Taarifa ya kwanza (case report 1)
Mwaka tisini na na sita, rafiki yangu mmoja, mtoto wake wa miezi mitatu alilazwa Muhimbili. Baada ya kuona maendeleo ya tiba si mazuri waliamua kumpima, majibu yakaonyesha ana virusi vya ukimwi. Majibu haya yalimfanya daktari aliyekuwa anamtibu mtoto kuwashauri wazazi nao wapime na wakakubli. Walipopima mama alikuwa mhathilika baba hapana, nawatu hawa walikuwa kwenye ndoa kwa muda wa miaka miwili, wakila tunda lao bila kinga.
Baada ya taarifa kufika kwa ndugu wa mwanaume wakashauri waachane wagawane walichochuma pamoja. Wakati wamepelekana mahakamani, mwanamke akana kwamba hawakuwahi kupima. Mahakama ikaamuru wapime, wakapima tena kwa hospitali chaguo la mwanamke. Majibu yakawa yale yale mama anao baba hana. Wakakubali kuachana na kugawana walivyochuma pamoja kama walivyoorodhesha mahakamani na baba kupangiwa kiwango cha kumlipa mama kwa malezi ya mtoto. Baada ya mwaka na nusu mtoto akapimwa tena na kugundulika hana ukimwi tofautu na alipokuwa amepimwa mwanzoni. Mpaka hapa ninapoandika wote wapo na afya njema, baba alioa mwanamke mwingine na wana watoto wawili na mama bado yupoanendelea kutumia dawa.
Uchunguzi usio rasmi ulionyesha mama alikuwa na ugonjwa huo hata kabla ya ndoa hiyo.
Taarifa ya pili
Jamaa yangu mmoja naye alikuwa ameoa na kualiwa watoto wanne katika ndoa yake. Ya miaka 15. Baadae  mwaka 2008 mke wake akaanza kuugua magonjwa ya ajabu ajabu, yanapona yanarudi na mapya yanajitokeza. Analazwa hospitali anaru tena baada ya muda, akaamua kwenda kwa mganga mpemba ambaye aliwambia mumewe ana mke mwingine kamtupia jini la damu. Akampa dawa hazikusaidia. Kutokana na lawama za hawala kuingia nabado hospitli na kwa waganga haponi, ikashauriwa wapime. Wakakubali. Walipopima mama anao baba hana. Mama akazidi kuamini kuwa hata kama ameonekana anaukimwi ametumiwa na huyo hawala wa mmewe. Ikawa kazi kumeza dawa, anaaza anaacha anakwenda kwa waganga wake, mara ya mwisho akaamua kuokoka sasa japo hapo kichwa nacho kilishaanza kuvurugika. Huko ndo kabisa akaambiwa aache dawa kabisa yesu atamponya. Mwanzoni mwa mwaka huu tumemzika.
Ninazo taarifa za namna hii nne lakini mbili zinatosha kutoa mjadala.
Mjadala
Katika taarifa zote mbili inaonyesha wahusika wote walishakaa pamoja wakila matunda yao bila kinga ndo maana wakapata watoto. Kwanini hawakuambukizana inawezekana walikuwa wanakula tunda lao bila michubuko yeyote katika kipindi chote walichokuwa pamoja. Sababu nyingine yawezekana wanaume hao wana kinga dhidi ya virusi vya ukimwi au chembe chembe zao za kinga hazina vipokezi (receptors) vya wadudu wa ukimwi. Tafiti zimeonyesha mdudu wa ukimwi huweza kuingia kwenye chembe chembe za kinga kupitia vipokezi katika hali ya kama ufunguo na kitasa au au nati na boriti. Kama mtu hana vipokezi hivi hawezi ambukizwa. Dr. Matthew Dolan, daktari bingwa katika jeshi la anga la marekani anasema, ansema Genetic resistance to AIDS works in different ways and appears in different ethnic groups. The most powerful form of resistance, caused by a genetic defect, is limited to people with European or Central Asian heritage. An estimated 1 percent of people descended from Northern Europeans are virtually immune to AIDS infection, with Swedes the most likely to be protected. One theory suggests that the mutation developed in Scandinavia and moved southward with Viking raiders.
All those with the highest level of HIV immunity share a pair of mutated genes -- one in each chromosome -- that prevent their immune cells from developing a "receptor" that lets the AIDS virus break in. If the so-called CCR5 receptor -- which scientists say is akin to a lock -- isn't there, the virus can't break into the cell and take it over. (haya yamenizengua kuyatafsiri)
Mtoto kuonekana ana ukimwi akiwa na miezi miatu na baada ya mwaka mmoja na nusu hana hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto anayezaliwa na mama mwenye virusi vya ukimwi huwa na antibodies dhidi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama yake. Unapopima ukimwi kutumia kipimo cha eliza ambacho uangalia antibodies hizi, basi mtoto huonekana hanao, lakini kama mtoto hakuambukizwa wadudu basi, antibodies hizi huondoka kwenye damu yake kadri muda unavyo kwenda.
Hitimisho
·         Kuna baadhi ya watu si rahisi kuwaambukiza ukimwi
Mapendekezo
  • Kutokupa  ukimwi kwa muda mrefu huku ukila tunda na mwenye nao kwa muda mrefu haikuhakikishii kuwa huwezi kuupata kwa hakikisha unafuata masharti ya kinga
  • Mtoto anayezaliwa na mama au wazazi wenye ukimwi si lazima awe nao fuata ushauri wa daktari na hasa kupima wakati wa ujauzito
  • Tuangalie namna ya kuwadhibiti waganga wa jadi na watumishi wa mungu wanashauri watu wasitumie dawa za kuongeza maisha