Saturday 10 December 2011

MATIBABU YA MZIZI WA JINO (ROOT CANAL TREATMENT)

Na Dr. Augustine Mbehoma Rukoma (DDS, MDent-restorative Dentistry)
Haya ni matiba ambayo hutolewa kwa jino ambalo sehemu ya uhai wake imearibika kiasi kwamba aliwezi kutibika kwa kuziba tu, kwa maneno mengine hii ndio njia mbadala ya kutibu jino bila kung’oa.
Matibabu huusisha kutoboa jino hadi sehemu ya uhai wa jino yenye mishipa ya damu na iliya ya fahamu na chembechembe za meno na kuviondoa nikimaanisha kuondoa mishipa ya fahamu, ya damu na chembe pamoja na ugonjwa na baadae kuijaza sehemu hii na vitu mahalumu vinavyokubaliana na mwili (biocompatible).
Aina za matibabu ya mziizi wa jino
Kuna aina kuu mbili za matibabu ya mzizi wa jino
1.      Nia ya kawaida (conventional root canal treatment)
Njia hii ni kama nilivyoeleza hapo juu, kuingia kwenye kiini cha jino na kuondoa kila kila kilichomo na kasha kujaza uwazi na vitu maalumu vinavyokubaliana na mwili
2.      Matibabu ya mzizi wa jino yanayohusisha upasuaji,
kwa njia hii mbali na kutumia njia ya kwanza, upasuaji hufanyika pia ili kondoa mfupa uliofunika ncha ya mzizi wa jino kusafisha eneo lililozunguka ncha ya mzii na baadae kukata ncha husika kasha kuziba kutokea kwa nyuma (retro grade filling). Njia hii hutumika pale njia ya kawaida inaposhindwa kuondoa tatitizo au inapoonekana kabisa kuwa haitaweza kuondoa tatizo. Huu ni upasuaji mdogo, unaofanyika kwa ganzi ndogo ya eneo husika (local anaesthesia). Mafanikio ya matibabu haya ni makubwa sana
Ni meno yapi yanahitaji matibu hayo
·         Meno yaliyooza hadi uoza kufikia kiini cha jino (dental pulp)-sehemu ya uhai wa jino.
·         Meno yaliyopata ajari na kupasuka na kuacha kiini cha jino kikiwa wazi (traumatic pulp exposure)
·         Meno yaliyopata ajari na kusababibisha mishipa ya damu kukatika au kubasuka na kuvujia ndani ya jino, kitu ambacho hupelekea jino kufa (pulp necrosis) na baadae kusabisha jibu au kubadilika rangi
·         Wahati mwingi japo ni mara chache, ni pale tunakuwa tunata kuliweka sawa jino/meno ambalo/ambayo hayakoo kwenye mstari sawa ili yaendane na menzake
·         Pia wakati mwingine, tunapo lisaga jino ili liweze kubeba meno bandia ya daraja (bridge) huku tukiwa na mashaka na uahi wake.
Nini dalili zinazo ashilia jino kuhitaji matibabu haya
·         Jino linalo uma- kuuma kwa jino kunashiria ugonjwa kuwa umeingia ndani ya kiini cha jino na au hata kupitiliza na kuingia kwenye mfupa ulioshikilia jino
·         Jino lililo oza na kusababisha uvimbe, liwe linauma au haliumi
·         Jino lililokatika na kupoteza zaidi ya nusu ya kichwa cha jino (crown) kukatika kuwe kwa hajari au kuoza au vyote kwa pamoja
·         Jino linalobadilika rangi huku kukiwa na historia ya kuligonga mahali au kuchapwa ngumi usoni, hapa jino linaweza kuanza kubadilika rangi miezi sita tangu siku ya ajari mpaka wakati mwingine hadi miaka ishiri wakati mgonjwa aliisha sahau hata hajari yenyewe
Meno yasiyo faa kwa matibabu haya
·         Meno yaliyoaribika vibaya kiasi kwamba hayatibiki tena japo ni machache, kwani hata kama jino limebaki mzizi tu, ukiwa bado imara twaweza fanya matibabu haya na baadae kujenga kichwa (crown)
·         Meno yaliyolegea sana kutokana na magonjwa ya fizi ambayo hayawezi kuimalishwa tena
·         Magego ya mwishi (wisdom teeth) kwa kawaida meno haya huwa yana maumbile yasiyotabirika kiasi kwamba hata mafaninio ya matibabu hayatabiriki, hii ikiambatana na kuwa yako nyuma sana kiasi cha kuwa vigumu kuyafikia kwa ufasaha na vifaa vyetu na pia yana mchango kidogo kwa usagaji chakula (2%)
·         Meno ambayo mifereji ya mizizi ambayo hupitisha mishipa ya fahamu na damu imeziba (calcified root canals)
Mafanikio ya matibabu haya
Kiwango cha mafanikio ya matibabu haya ni kati ya asilimia sabini na saba hadi tisini na nane (77-98%)
Haya ni mafannikio ya hali ya juu kwa matibabu ya aina yeyote ile, mafanikio uongezeka zaidi pale tabibu anapotumia vifaa vya kumuongezea uwezo wa kuona kama dental loops na operating microscope.
Kutokufanikiwa kwa matibabu haya
Ziko sababu mbali mbali zinazoweza kusababisha matibabu haya yasifanikiwe, baadhi zikitokana na udhaifu wa tabibu na zingine kutokana na jino lenyewe lilivyo (internal tooth morphology)
Tabibu-tabibu kama hakusafisha jino vizuri na kuliziba sawasawa upo uwezekano mkubwa wa matibabu haya kutokufanikiwa, pia tabibu kama hajui maumbili ya ndani ya jino vizuri, kuna uwezekana sehemi zingine kuachwa bila kusafishwa.
Meno –meno mengine yana maumbile yasiyo ya kawaida, mfano katika hali ya kawaida meno ya mbele yana mfereji mmoja wa kupitisha mishipa ya fahamu na damu, lakini kuna jino linguine linakuwa na miwili au mitatu, hapa kwa mazoea na kwa kukosa vifaa vya kisasa ni rahisi kusafisha mfereji mmoja na kuacha mingine, vivyo hivyo kwa magego ambayo kwa kawaida yana mifereji mitatu hadi mine, lakini mengine mitano, sita, saba hata utafiti Fulani huko china umegundua badhhi ya magego kuwa na matundu nane, meno ya namna hii ni vigumu kufanikiwa.
Nini kifanyike ili kupunguza uwezekano wa matibabu kutokufanikiwa?
Tabibu lazima ajikumbushe maumbile ya ndani ya jino analotaka kulitibu kabla ya kuanza matibabu na pia ajue kwamba jino laweza kuwa na mifereji ya ziada hivyo ajitahidi kuitafuta.
Matumizi ya vifaa vya kusaidia kuona ni muhimu na hata matumi ya x-ray za kisasa kama 3 dimensional digital x-ray ili kuweza kuona pande tatu za jino
Kwanini meno yanendelea kutolewa wakati matibabu haya yapo?
·         Matibabu haya ni gharama ukilinagisha na kung’oa jino hii ikienda pamoja na umaskini wa wananchi walio wengi, wanashindwa kuyagharamia na hivyo kuchagua kung’oa
·         Baadhi ya hospitali hazina wataalamu au vifaa vya matibabu haya au vyote kwa pamoja
·         Mwamko mdogo wa wananchi kuhusu matibabu ya meno, hii inachangiwa pia na tabibu wa meno kutokuelezea matibabu mbadala zaidi ya kung’oa, tafiti zimeonyesha baathi tabibu wa meno hutoa maelezo kwa yale matibabu wanayoyaweza tu, badala ya kuwaeleza pia upatikanaji wa matibabu mbadala katika sehemu zingine
·         Watu kuchelewa kufika hospitalini, wakija baadhi yao matibabu pekee yanayo kuwa yamebaki ni kung’oa tu, hapa napo kuna mchango wa umaskini na uelewa mdogo
·         Imani potofu kuwa tiba ya kudumu ya jino ni kuling’oa
·         Uzoefu wa zamani, kwa mtu ambaye aliwahi kuziba jino na likauma tena, ukimwambia matibabu haya ni vigumu kuyakubali
Hitimisho
·         Jali meno yako kama unavyojali viungo vingine vya mwili wako
·         Kungoa jino kama tiba ya ugonjwa wa jino, ni pale tu ambapo jino hilo haliwezi tibika kwa njia mbadala kama hii ya mzizi wa jino au pale inapobainika kuwa jino husika kuendelea kubaki pale hata likiwa limetibika linaweza kuwa chanzo cha kuleta madhara makubwa mwilini kama uoto mpya n.k.