Friday, 14 October 2011

KULIKA KWA MENO (TEETH WEAR)

Na Dr. Augustine Mbehoma Rukoma
Hii ni hali ya ambapo sehemu ngumu ya nje ya meno uondoka na kusababisha sehemu ya ndani kuwa wazi. Tatizo hili huanza kwa kuondoka sehemu ngumu ya nje (enamel) na kuiweka wazi sehemu ya kati ambayo ni ngumu pia (dentine). Tatizo likiendelea bila matibabu hufanya kiini cha jino ambako kuna mishipa ya damu, mishipa ya fahamu na chembe chembe mbali kuwa wazi (dental pulp exposure).
Dalili hutegemea na kiwango cha ulikaji. Kama ni sehemu ya nje kabisa imetoka, dalili uweza kuwa msisimuko (sensitivity) wakati wakunywa vinywaji vya baridi, vya sukari na hata upepo ukiyapuliza meno. Kama kiini cha jino kitakuwa wazi basi maumivu uanza na yanaweza kuwa makali kabisa.
Matibabu hutegemea kiwango cha uharibifu. Kama uharibifu ni kidogo utumiaji wa dawa za meno zenye madini zaidi hasa ya fluoride (magaddi?) inaweza kuondoa dalili, wakati mwingine kutumia dawa za kupaka kitaalam, kuziba na kuvalisha kofia ngumu (crown) meno husika na mwisho ni kufanya matibabu ya mzizi wa jino (root canal treatment) au kung’oa jino kama kiini cha jino kimebaki wazi.
Ziko aina mbali mbali za kulika kwa meno kutokana na nini kinasababisha tatizo, na kinga au tiba hutegemea nini kisababishi.
Kusagika kwa meno (attrition)
Huku ni kulika kwa meno kwenye sehemu ambapo meno ya juu na chini hukutana (occlusal surfaces). Katika hali ya kawaida meno hulika sehemu hizi kutokana na kadri yanavyoendelea kutumika kusaga vyakula, hali hii uendelea polepole kadri mtu anavyoendelea kuishi (umri) kitaalamu inajulikana kama phyisiological attrition. Si rahisi kuhisi dalili zake kwani mwili hujaribu kuzipa vitundu vya mifereji midogo inayotoka kwenye kiini cha jino kwenda kwenye sehemu ngumu ya kati (dentine). Ni vitundu hivi ambavyo vikiwa wazi husababisha msisimko (sensitivity). Kulika kwa meno sehemu ya kusaga unakuwa ugonjwa pale unapotokana na mambo mengine zaidi ya kule kwa kawaida kwa kuongeza umri
Baadhi ya matatizo yanayosababisha hali
1.      Kusaga meno (bruxism)- hii ni hali ambayo mtu husaga meno yake wakati hatafuni kitu chochote na mara nyingi mtu huwa hajitambui kama ana tatizo hili. Hali hii mara nyingi hujitokeza wakati wa usiku mtu akiwa amelala (nocturnal bruxism) japo kwa wachache wanaweza saga mchana pia. Si rahisi mtu wa namana hii kujitambua mpaka pale atakapoambiwa na mtu wanayelala pamoja au atakapo kwenda kwa mtaalamu wa meno na kuelezwa.

Nini husababisha hali hii
Yapo baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha tatizo hili na zaidi inahusishwa na mabadiliko ya ki saikologia. Watu wenye mawazo mengi wanaonekana kuwa kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili.

Tatizo hili pia linaweza kutokana na jino lililozibwa na kujazwa zaidi ya kwaida. Mwili hufanya harakati za kupungu sehemu ilyozidi kwa kuisaga na hatimaye kujikuta umejenga mazoea, kiasi kwamba hata jino likisha kuwa levo bado unaendelea kusaga tu.

Pia wale wanaokaa kwenye meza kwa muda mrefu wakisoma au vyovyote huku wameshikiria kidevu kwa nguvu, nao ni wahanga wa ungonjwa huu. Katika hali ya kawaida mtu ukiwa umefunga mdomo umetulia meno ya juu na ya chini huwa hayakutani bali huacha nafasi kama milimita mbil hivi (resting space). Sasa ukiyabana pamoja kwa muda mrefu kwa kushikilia kidevu, utayafanya yajenge mazoea kuyakushikana hata pale ambapo hujashika kidevu na mwishowe kuanza kusagana

Dalili zake na viashilia vyake ni mgonjwa mwenyewe kuhisi msisimko wakati wa kunywa vitu vya baridi, maumivu kama kiwango cha uharibifu ni kikubwa kiasi cha kukiacha kiini jino wazi (dental pulp exposure). Ukiangalia meno utakuta yamelika sehemu ya kutafunia kwa magego na visaidizi vyake (molars and premolars), sehemu sa kukatia na kuchoma kwa meno ya mbele (canines and incisors). Kusagika huanzia sehemu za meno zilizoinuka (cusps) ambazo hatimaye huondoka kabisa na kuwa flati. Meno huweza kusagika mpaka wakati mwingine kufikia kwenye levo ya fizi. Watu wenye tatizo hili huonekana wana uso wa mraba kutokana na msuli mkubwa wa kuvuta taya (masseter muscle) kunenepa kutokana na kutumika zaidi. Mgonjwa pia huweza kuchoka kirahisi misuri wakati wakutafuna katika hali ya kawaida.
Tatizo linaweza kuathili hata sehemu ya muunganiko wa taya la chini na fuvu (tempromandibular joint-TMJ). mgonjwa huweza kusikia maumivu kwenye jointi hii na wakati mwingine kufyatuka fyatuka (TMJ dislocation) au kutoa sauti wakati wakufungua na kufunga kinywa (popping or cricking sound in TMJ).












Picha zikionyesha meno yalisagika



Kwa chini; upande wa juu-kinachoonekana kama kuvimba shavu ni msuli wa kuvuta taya (masseter muscle) ulioongezeka ukubwa kutokana na kusaga meno. Picha ya chini mwezi mmoja baada ya kupata matibabu ya uhakika, msuli unarudi katika hali ya kawaida.

Matibabu –ni vizuri kujua chanzo cha tatizo hili na kukishughulia kwanza kabla ya kufanya matibabu zaidi ya meno kurekebisha uharibifu uliotaka na msagiko. Utafiti unaonye wengi wenye matatizo haya ni wenye mawazo yaliyo zidi kiwango (stress). Lazima hujue kwanini mtu anawaza sana ili umkancell au hata umpeleke kwa wataamu wa mambo hayo (psycologist) ili waweze kumsaidia.

Wakati hayo yakiendele inabidi kumfundisha mgonjwa kulegeza taya (relaxation exercise) na kuachanisha meno kila anapo hisi meno ya juu na ya chini yamekutana. Akifanya mazoezi haya kwa muda mrefu mwili huweza kujenga mazoea kuwa kila meno yakikutana yaachanishwe (conditioned reflex action). Mgonjwa akiacha kusaga basi matibabu ya kurekebisha madhara yanaweza kufanyika kwa mafanikio makubwa, iwe kuziba, kuua mzizi wa jino na kuyavalisha meno kofia ngumu hasa metal reinforced porcelain crown
Kwa wale ambao ni vigumu kuacha tabia ya kusaga wanaweza kutengenezewa kifaa maalumu cha kulinda meno wakati wa usiku (nigh guards), mgonjwa anava kifaa hiki usiku wakati wa kulala kuzuia meno kugusana na baada ya muda atazoea pia na kuacha kusaga. Kifaa hiki husaidia pia kuondoa matatizo yaliyokwisha jitokeza kwenye jointi.         
                                                                  


kifaa cha kukinga meno                                mgonjwa akiwa amevaa kifaa
yasisagane (night guard)


Ni vizuri kumuuliza mwenzako kama amewai kukusikia ukisaga meno usiku ili uweze kuchukua hatua za kuwaona wataamu mapema. Kumbuka kujua tatizo mapema na kulitibu ni sehemu ya hatua za kinga.

No comments:

Post a Comment