Friday, 14 October 2011

Kuoza kwa meno (Dental Caries) ni ugonjwa wa kuambukiza

Dr. Augustine Mbehoma Rukoma 
Miaka ya nyuma iliaminika ugonjwa wa kuoza kwa meno si wa kuambukiza; lakini tafiti nyingi zilizofanyika zimethihilisha ni ugonjwa wa kuambukiza. Jino lililooza linaweza kuambukiza meno yaliyogusana nalo na pia mgonjwa aliyeoza meno au mwenye wadudu wanaosababisha kuoza kwa meno anaweza kuambukiza mwenzake/wenzake.
Wadudu wanaosababisha kuoza kwa meno ni sehemu ya wadudu wakazi kinywani (oral flora). Wadudu hawa hujishikiza kwenye meno na kufanya utando, wana uwezo wa kuchachua vyakula hasa vyenye asili ya sukari na kutoa tindikari. Ni tindikali hii ambayo huvuta madini kwenye meno na kuweka matobo. Utando huu wa wadudu kwenye jino moja unaweza kuwa na wadudu nusu biliononi, miongoni mwake ikiwemo jamii ya  mutans streptococci ambao kimsingi ndio wasababishaji wakuu wa kuoza meno. Waduduwengine ni kama Lactobacillus na Actinomyces
Namna ya kuambukiza-ndani ya jamii ya wadudu hawa ziko jamii zingine ndogondogo ambazo zinatofautiana kwa uwezo kuchachua vyakula na kutoa tindikali na hata uwezo wa kujishikiza kwenye meno. Kwa mtu mwenye wadudu wasio wakali anaweza kuambukizwa na mwenzake mwenye wadudu wakali na hivyo kuingia kwenye hatari zaidi ya kuoza meno. Tafiti zimeonyesha wapenzi/wanandoa kwa njia ya kubusiana wanaweza kuambukizana kwa njia hii. Watoto wanaochangia ice cream/ice water mashuleni pia wanaambukizana kwa njia hii. Tafiti pia zimeonyesha wazazi wanaotafunia vyakula watoto wao kama sehemu ya kuvilainisha wanaambukiza pia.
Njia nyingine ni jinolililooza kuambukiza menzake linayogusana nayo, tindikali inayozalishwa na wadudu katika jio lililooza linaweza kuathili lililo jirani. Ndio maana inashauriwa ukiona jino limeanza kuoza muone mtaalamu akalitibu au akaling’oe kama alitibiki ili lisiambukize mengine.
Namna ya kujikinga-
·         Njia muhimu ni kutembelea cliniki za meno angalau kila baada ya miezi sita
·         Kuzuia watoto kuchangia vyakula mudomoni
·         Kupima kuangalia kiwango na aina za bakiteria zilizi kwenye mate yake na kupata dawa ikibidi.
·         Kuhusu kubusiana sina la kusema

No comments:

Post a Comment