Friday, 14 October 2011

MATIBABU YA MENO YALIYOJIPANGA VIBAYA (ORTHODINTIC TREATMENT)

Baadi ya watu wana meno yaliyojipanga visivyo. Katika hali ya kawaida meno yanatakiwa yawe katika mahusiano mazuri kiasi kwamba meno ya juu yaweze kukutana vizuri na yaliyo jirani yakae vizuri pia. Utakuta baadhi ya watu meno ya juu yamechomoza mbele sana kiasi kwamba hata kufunga mdomo ni tatizo, wengine ya chini kuvutika mbele zaidi na kuwa na kidevu kilichochongoka kwenda mbele na wengine yamepandana pandana. Mpangilio mbaya wa meno unaweza kuwa mbaya zaidi kiasi cha kumugasi mhusika na wakati mwingine meno yenyewe kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Taizo linguine la meno yalijipanga vibaya ni vigumu kuyasafisha na hivyo kuyaweka meno katika hatari ya kuoza na kusababisha magonjwa ya fizi.
Nini kinasababisha matatizo haya?
·         Maumbili yatokanayo na vinasaba na uridhi
·         Tabia kama kunyionya vidole utotoni hata ukubwani kwa wengine
·         Kuwahi kutoka meno ya utotoni
·         Kuchelewa kutoka kwa mano ya utotoni hivyo kuyafanya ya ukubwani kuota upande
·         Ajari wakati wa kujifungua ambayo inaweza kuadhiri maeneo ya kukua kwa taya
Matibabu-lengo kubwa la matibabu ni kuyaweka meno katika mpangilio unaokubalika, ili kuboresha muonekano, utafunaji na hata utamkaji wa maneno.
Matibabu huusisha kuwekewa nyaya kwenye meno ambazo husaidia kuyavuta na kuyaweka katika mpangilio mzuri. Nyaya zaweza kuwa za kufunga moja kwa moja kwa vifaa maalumu na kuwa vinafanyiwa marekebisho kadri meno yanavyozidi kujipanga (fixed orthodontic appliances); lakini pia nyaya hizi zaweza kuwa za kuvaa na kuondoa kadri mgonjwa anavyotaka (removable orthodontic appliances). Kama mpangilio ni mbaya zaidi, ili kufanikisha matibabu haya, yawezekana baadhi ya meno kuondolewa ili kutoa nafasi kwa yaliyobaki kujipanga.
 Muda wa kuvaa nyaya hizi yaweza kuwa miezi sita au zaidi kulingana na ukubwa wa tatizo na wakati mwingine ushirikiano wa mgonjwa.
Muda mzuri wa kufanya matibabu haya ni pale ambapo mtoto bado anakuwa anakua (chini ya miaka 18). Zaidi ya umri huu matibabu huwa magumu, kuchukua muda mrefu na wakati mwingine kutoa matokeo ambayo hayaridhishi.
Kwa wale ambayo matatizo haya yanatokana na mojawapo ya mataya kuwa dodo kuliko kawaida au kunyume chake basi upasuaji unatakiwa kupunguza au kuongeza taya husika.
Ni vizuri kuwaangalia watoto wetu mara kwa mara, kwani matibabu ni rahisi yakigundulika mapema.
Msisitizo tembelea kliniki ya meno wewe pamoja na familia yako angalau mara mbili kwa mwaka. Kumbuka matibabu ya meno ni gharama na bima nyingi zinayakimbia. Tiba ya mapema ni sawa na kinga.
Picha hapo chini zinaonyesha mgonjwa kabla, wakati na baada ya matibabu
Kabla ya matibabu
Wakati wa matibabu


Baada ya matibabu

10 comments:

  1. Mimi mwanangu jino la utoto lilitoka lilipofika mda wake lilitoka likaota lingine vizuri lakini lililoota bahati mbaya alianguka likakatika robo je kunauwezekano Wa hicho kipande kilichobaki kutolewa na kuota lingine??

    ReplyDelete
  2. Dr naomba namba ako ninatatizo kubwa la meno

    ReplyDelete
  3. Doctor kuna uwezekano wa kung'oa yaliyo pandiana ukiwa na miaka 25?

    ReplyDelete
  4. Doctor naomba kujua being ya kupanga meno ya juu tu,tafadhali naomba kujua

    ReplyDelete
  5. Habar doctor,naomba kufaham unapopatikana au namba za mawasiliano tafdhar, Nina mtoto Ana shida hiyo..
    Asante

    ReplyDelete
  6. Doctor naomba namba yako nina tatizo la meno

    ReplyDelete